Waheshimiwa Madiwani wilaya ya Kyela wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa ziara za kutembelea na kukagua miradi kwa kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 10/08/2023, ikijumuisha Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu, Gasper Mwanandeje akiwa na wataalamu kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wametembelea Mradi wa uzalishaji wa miche bora ya michikichi katika ofisi za halmashauri kata ya Bondeni wenye gharama ya shilingi 16,594,000, mradi wa ujenzi wa zahanati katika kata ya Ndandalo wenye thamani ya shilingi 155,000,000, Ujenzi wa shule Mpya kata ya Njisi yenye thamani ya shilingi 347,500,000, Ujenzi wa mradi wa maji Lema wenye thamani ya shilingi 415,439,846.22 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja katika kata ya Mababu wenye thamani ya shilingi 161,657,445.
Miradi yote iliyotembelewa, kukaguliwa na kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, imeridhiwa na waheshimiwa madiwani ikiwa ni pamoja na kutoa pongezi zao za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta fedha nyingi zinazotekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya Kyela.
Aidha waheshimiwa madiwani wametoa maagizo ikiwemo agizo la umaliziaji wa miradi ya maendeleo kwa muda uliyopangwa.
Hayo yote yamepokelewa na timu nzima ya wataalamu wa halmashauri pamoja na Taasisi za serikali wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Gasper Mwanandeje.
Ziara za kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa robo ya nne 2022/2023, umekamilika.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa