Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango Miji ya Mamalaka ya Mji Mdogo Kyela imefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la kupumzikia abiria katika stendi kuu ya Mabasi Kyela tarehe 28.05.2025
Aidha mradi huo umegharimu kiasi cha Tsh.17,500,000/= Mpaka sasa kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Jimbo umetoa Tsh.7,000,000/= Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imetoa Tsh.500,000/= Pamoja na Ofisi ya Mamlaka ya Mji mdogo imetoa kiasi cha Tsh.10,000,000/=
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati,Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka Lutamyo Mwasipu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwajali Wananchi wake kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mhe.Mwasipu ameitaka kamati za ujenzi kuzingatia usafi wa mazingira katika maeneo ambayo miradi ya maendeleo inatekelezwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa