Kamati ya siasa Mkoa wa Mbeya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mhe.Patrick Mwalunenge imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi tarehe 14.5.2025.
Miradi iliyotembelewa ni Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Mbeya iliyogharimu Shillingi billion 4,906,785,794.00,jengo la mama na mtoto lililopo kituo cha Afya Kilasilo ambacho Limegharimu Million 680,000,000 pamoja na jengo jipya la Utawala la Halmashauri ambalo mpaka sasa limegharimu Millioni 820,000,000,na ujenzi bado unaendelea.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Mhe. Mwalunenge Amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali Wananchi wa Wilaya ya Kyela kwa kuleta fedha za kuanzisha na kuendeleza miradi ya maendeleo.
Mhe.Mwenyekiti ameupongeza uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa ushirikiano mzuri wa usimamizi wa miradi na kuhakikisha shughuli mbalimbali za maendeleo zinafanyika kwa wakati,na ubora na wananchi wanapata huduma sahihi.
Aidha Mhe.Mwalunenge amewataka Waganga wa Hospitali na vituo vya Afya kusimamia Miundombinu iliyopo katika vituo vya kutolea huduma hizo na kuhakikisha Wagonjwa wanapata huduma nzuri.
Kuhusu suala la ukosefu wa ajira ambayo imekua ni changamoto kwa Vijana wanaohitimu masomo ya Elimu ya juu Mhe.Patrick Mwalunenge amewataka wataalamu na Mwenyekiti wa Halmashauri kubuni miradi ili Vijana hao waweze kujikita na uzalishaji wa mazao mbalimbali yatakayoweza kuwapatia kipato cha kukidhi mahitaji yao.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilan Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ,kwa kutatua kero za wananchi wa wilaya Kyela kupitia fedha zinazoletwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mfumo mzuri wa bei katika sekta ya kilimo hususani kwa zao la biashara la kokoa kwani Halmashauri pamoja na Wananchi wananufaika kupitia zao hilo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa