Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kyela Mheshimiwa Patrick M.Mwampeta(alievaa kofia) akiongea na baadhi ya wananchi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Itunge.
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kyela, imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo hapa wilayani, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya chama inayowataka kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo ili kijiridhisha na kasi pamoja na ubora wa miradi hiyo.
Ujenzi wa shule ya mchepuo wa kingereza katika kata ya Njisi bado unaendelea kwa kasi kubwa.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 27/01/2022 kwa kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa kituo cha Afya Itunge kilichopo katika kata ya Itunge, kikundi cha akina mama "Tupendane" kikundi kinachojishughulisha na ukamuaji wa mafuta ya mawese, kikundi cha watu wenye ulemavu kilichopo kata ya Bondeni, kikundi kinachojishughulisha na bodaboda.
Wajumbe wa kamati ya siasa Kyela wakiongea na wanakikundi cha watu wenye ulemavu katika kata ya bondeni.
Ujenzi wa mradi wa wodi ya mama na mtoto katika hospital ya wilaya ya Kyela, ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa vilivyojengwa kwa kupitia mradi namba "5441TCRP" ambapo wameweza kufika katika shule ya sekondari Ipinda pamoja na mradi wa ujenzi wa kutuo cha Afya katika kata ya Makwale.
Kituo cha Afya Makwale mafundi wakiendeleza ujenzi.
Aidha Mwenyekiti wa Chama Tawala Kyela Mheshimiwa Patrick M. Mwampeta amesema, kazi zinazofanywa na wanaKyela kwa sasa zinafaa kuigwa kwani wananchi wa Kyela wamekazana katika kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo hapa wilayani. Pia alitoa pongezi nyingi kwa wananchi wa kata ya Itunge kwa kusimama kwa pamoja na kuukamilisha mradi wa kituo cha Afya kwa asilimia kubwa.
Pia Mheshimiwa mwenyekiti hakusita kutoa pongezi zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa mkoa wa Mbeya , Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi pamoja na watalaam kwa umoja wao na moyo wao wa kujitoa hadi kusababisha kuleta maendeleo chanya katika wilaya ya Kyela kwa sasa.
Muonekano wa kituo cha Afya Itunge kwa sasa, kituo kilichotembelewa na kamati ya siasa ya wilaya.
Nae diwani wa kata ya Itunge Mheshimiwa Nikson Mwalukama alitoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya 6, kwani kwa kipitia fesha kiasi cha shilingi milioni 250 zilizotolewa na serikali, zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha afya. Pia aliongeza kwa kusema wananchi wa kata hiyo bado wananguvu ya kutosha kukamilisha mradi huo pamoja na kupokea mradi mwingine wowote katika kata yao kwa maendeleo ya wanakyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa