Kamati ya Siasa ya wilaya ya Kyela imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo leo tarehe 23/08/2023.
Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kyela Mhe. Elias Mwanjala akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, Wakuu wa idara, vitengo pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimbali.
Kamati imetembelea mradi wa Maji wa Mbambo - Kyela ambapo shughuli ya kutandika mabomba imeanza, Mradi wa Umeme (REA) katika kata ya Lusungo, ujenzi wa kituo cha afya kata ya Makwale, Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Matema, pamoja na mradi wa Ufugaji nyuki katika kata ya Talatala.
Aidha mradi wa ufugaji nyuki kata ya Talatala una wafugaji nyuki 22 ambapo kuna wafugaji binafsi na vikundi kwa umoja wao, wanamiliki mizinga zaidi ya 300.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela imekuwa ikiwasaidia wafugaji hao, kwa kuwapa elimu, ushauri na kuwagawia vifaa vya urinaji asali.
Wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya wametoa pongezi nyingi kwa wataalamu kutokana na usimamizi mzuri wa miradi yote waliyoitembelea.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa