Mwenyekiti wa chama tawala (CCM) Mkoa wa Mbeya(kushoto) Mhe. Solomon J. Itunda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (kulia), Mhe.Albart Chalamila, wakiwa wametoka kukagua kituo cha zahanati kilichopo kijiji cha Kyangala kata ya Talatala wilayani Kyela.
Kamati ya siasa ya Mkoa wa Mbeya ikiongozwa na mwenyekiti wa chama tawala (CCM) Mhe. Solomon J. Itunda, imefanya ziara ya kikazi hapa wilayani Kyela siku ya jana tarehe 20/01/2020.
Katika ziara hiyo kamati imepata fulsa ya kutembelea miradi mutatu yaani mradi wa utengenezaji wa bidhaa za asili mfano sabuni zitokanazo na mafuta ya mawese, vikapu vya shanga na bidha nyingine nyingi, mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kyangala iliyopo kata ya Talatala wilayani Kyela, pamoja na mradi wa Maji(Kapapa) uliyopo kijiji cha kingili kata ya Ipinda hapa Kyela.
Akizungumza na Wananchi wa kata ya Taratara wilayani hapa, Mwenyekiti wa cha tawala (CCM) Mhe. Solomon J. Itunda amesema, kazi kubwa ya Waheshimiwa madiwani ni kutoa ushauri wa uanzishwaji wa miradi inayotekelezeka ili kuweza kuisaidia jamii husika na kufanisha sera ya chama pamoja na nchi kwa ujumla wake.
Pia Mhe. Solomon J. Itunda alisema viongozi wajitahidi kukamilisha miradi kwa wakati na ikibidi wachague miradi michache ambayo inaweza kukamilishwa kwa asilimia 100 ili kuwafanya wananchi kunufaika na miradi inayoanzishwa katika maeneo yao.
Aidha Mhe. Itunda alitoa maelekezo kwa viongozi wa chama na Serikali kwamba, viongozi wote kukaa pamoja na kukubaliana kutekeleza miradi ambayo itaanzishwa na kuikamilisha kwa wakati na kwa manufaa ya wananchi wote.
Kwa ujumla wananchi wa wilaya ya Kyela wamezipongeza jitihada zinazofanywa na viongozi wa serikali ya awamu ya tano, kwa kufwatilia na kutoa huduma za kutosha kwa wananchi wa Tanzania.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa