Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Livingstone Mwangalaba wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo tarehe 15.5.2025.
Miradi iliyokaguliwa ni Kyela Cocoa Girls ambayo mpaka sasa imegharimu fedha ni Tsh.195,000,000.00/=,kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Tsh. 165,000,000.00 ikiwa ni fedha kutoka mfuko wa Kakao pamoja na Tsh. 30,000,000.00 kutoka tasisi ya Tulia Trust
Mradi mwingine ni kikundi cha Vijana cha wauza kuku Matenki kilichokopeshwaTsh.20,000,000/= (Milioni ishirini) kilichonufaika kupitia mkopo wa 10%, zinatolewa na Halmashauri.
Hata hivyo Kamati imekitaka kikundi cha Vijana cha wauza kuku Matenki kukuza mtaji wao kupitia biashara hiyo na kuwa waaminifu katika urejeshaji wa fedha walizokopeshwa ili waweze kukopa kwa mara nyingine.
Aidha kamati ilienda kukagua Shamba la Michikichi la Mkulima lenye ekari 3.5 lililopo Kata ya Ikimba. Ambapo Miche hiyo ya Michikichi ni Mbegu Bora inayooteshwa na Idara ya Kilimo na kugawiwa wakulima Bure.
Sambamba na hayo Wah.Madiwani wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruzuku za mbegu za kisasa zinazozalisha Michikichi inayogawiwa bure kwa Wananchi.
Aidha Kamati imeshauri Uongozi wa Shule kuandaa eneo kwa ajili ya kupanda miche ya Cocoa ili kuleta maana halisi ya jina la Shule.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa