Kamati ya ukaguzi na Tathimini ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kyela, pamoja na baadhi ya wananchi katika shule ya Sekondari Busale ambapo ziara yao ilianzia hapo.
Kamati ya ufuatiliaji ujenzi wa madarasa yanayojengwa kwa kupitia “mradi namba 5441 Tanzania COVID 19 Social-Economic Response And Recovery Plan”(TCRP),imefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa tarehe 12/01/2023 katika halmashauri ya wilaya ya Kyela,
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa katika shule ya Sekondari Busale Kyela.
Kamati hiyo imejuisha wajumbe watatu yaani, ndugu Emmanuel Kilundo (Kaimu Ras Mkoa wa Mbeya), George Joseph Mringay (TAMISEMI), pamoja na Ndugu Iddy Said kutoka Wizara ya Fedha. Ambao kwa pamoja wameweza kutembelea na kufanya tathimini ya ujenzi wa madarasa hayo na kuridhishwa na kazi nzuri ya ujenzi wa madarasa hayo.
Mmoja kati ya wanakamati ya ukaguzi na tathimini, Ndugu George Joseph Mringay akiwa ameketi katika moja ya madawati mazuri yaliyotengenezwa katika shule ya Sekondari Ikama. Kazi ya Ukaguzi na Tathimini ikiendelea katika shule ya Sekondari Nkuyu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa