Kamati ya Ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo miradi inayotekelezwa na serikali pia miradi inayotekelezwa na watu binafsi.
Lengo la ziara ni kujua jinsi miradi ya serikali inavyotekelezwa kwa wakati, pia kujua mchango wa miradi binafsi kwa Wananchi.
Ziara imefanyika tarehe 18/05/2024, Mkurugenzi Mtendaji Bi. Florah Luhala akiwa ni mmojawapo wa wajumbe walioambatana na kamati hiyo, wakiwemo na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa Kituo cha Afya Itunge( Jengo la mama na mtoto), Kituo cha afya Ngonga, Mradi wa barabara kata ya Mwanganyanga, shamba la mkulima wa kakao kata ya Ndandalo, Kikundi cha wanawake wanaoishi katika makundi hatarishi(DREAM'S), pamoja na kiwanda cha kutengeneza mafuta safi ya kula kwa kutumia michikichi kata ya Itope.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa