Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya tarehe 21-22/08/2023, imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo, itakayopitiwa na mbiyo za Mwenge wa Uhuru tarehe 08/09/2023 wilayani Kyela.
Kamati imeongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, akiambatana na Wakuu wa Idara, vitengo na wakuu wa Taasisi.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa maji kijiji cha Lema kata ya Busale wenye thamani ya shilingi 415,439,846.22, Mradi wa ujenzi wa shule mpya Kirambo kata ya Njisi wenye thamani ya shilingi 347,500,000, Mradi wa upandaji miti katika shule mpya ya msingi Kilambo, Mradi wa kitalu cha michikichi kata ya Bondeni.
Miradi mingine ni pamoja na kikundi cha vijana Madereva waendesha magari aina ya Noa 2, ambazo walizipata baada ya kukopeshwa mkopo wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kutoka halamashauri ya wilaya, mradi wa ujenzi wa zahanati ya Ndandalo kata ya Ndandalo pamoja na mradi wa Ujenzi wa daraja kata ya Mababu wenye thamani ya shilingi 161,657,445.
Kamati imetoa maelekezo na Ushauri kwa miradi iliyotembelewa, Mkuu wa wilaya ya Kyela amepokea ushauri kwa niaba ya wataalamu na kuahidi kutekeleza yote yaliyoshauriwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa