Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya tarehe 06/12/2023, ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo wilayani Kyela, pia amepata fulsa ya kuongea na kusikiliza kero kutoka kwa watumishi wakiwemo watendaji wa kata, vijiji pamoja na Wakuu wa Idara.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa bweni la wanafunzi Kiwira coal mine (KCM), Shule ya msingi Mjimwema kata ya Ikimba, shule ya msingi Kilambo kata ya Njisi na ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa katika kata ya Busale.
Akiongea katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Katibu Tawala Mkoa Ndugu, Rodrick Mpogolo ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi. Florah A. Luhala, viongozi watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi, lakini amewataka watendaji wa kata na vijiji, kusimamia miradi yote ambayo imeanzishwa katika kata zao na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.
Pia amewataka watendaji wakata kuhakikisha wanawabaini na kuhakikisha watoto wanaotakiwa kuandikishwa shule waandikishwe na pia wanafunzi waliofaulu darasa la saba katika kata zao wanakwenda kidato cha kwanza ifikapo mwezi wa kwanza 2024.
Vilevile amewataka watendaji kuhakikisha shule zao zote zinamadawati na tayari kwa kupokea wanafunzi.
Kwa upande wa Afya amewataka wataalamu kusimamia suala la usafi, kwani kwa kipindi hiki mvua zinaanza na wilaya ya Kyela ni wilaya ambayo huwa inakumbwa na ugonjwa wa kipindupindu, hivyo amewaomba viongozi kusimamia suala la usafi.
Mwisho aliwataka watendaji kusimamia Ulinzi na usalama pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa