Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Lodrick Lazaro Mpogoro, amefanya ziara katika wilaya ya Kyela na kupata fulsa ya kuongea na watumishi wa serikali ndani ya Ukumbi wa Halmashauri hapa wilayani Kyela, ziara hii imegusa masuala ya kukumbushana taratibu, kanuni za kazi katika utumishi wa umma. Ziara hii imefanyika leo tarehe 24/11/2022.
Aidha Ndugu Mpogolo amesema, amekuja kujitambulisha lakini pia kuwaunganisha watumishi wote wanaofanya kazi wilayani na wale wanaofanya kazi Mkoani. Amewataka watumishi kufanya kazi kwa pamoja kwa kufuata kanuni na tarazibu za utumishi wa umma. Pia amewasihi watumishi wanaofanya kazi Mkoani kuwa karibu na wale wanaofanya kazi wilayani, kwani kwa kupitia umoja huu maendeleo yatapatikana kwa kasi zaidi ya hapa tulipo.
Amesema mafanikio yoyote yale ya kimaendeleo katika nchi yanatokana na wataalam kwa kutimiza majukumu yako, lakini kufanya kazi kwa kuheshimiana. "Mkuu wa Idara yeyote ambae atamdharau msaidizi wake huyo hatufai katika Mkoa wa Mbeya" alisema Ndugu Mpogolo.
Pamoja na hayo, Mheshimiwa Katibu tawala Mkoa amewapongezi wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kufanya kazi vizuri na kusimamia miradi ya maendeleo inayoshamiri katika wilaya ya Kyela.
Wakati huo huo ndugu Mpogolo, ameipongeza Halamashauri ya wilaya ya Kyela kwa ukusanyji mzuri wa mapato, maana hadi kufikia sasa Kyela ni Halmashauri ya 3 ikiongozwa na Halmashauri ya Chunya, Busokelo kwa ukusanyaji wa mapato.
Akimaliza kutoa ujumbe wake Ndugu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, amewaasa watumishi kuachana na ulevi wa pombe kwani kunywa hadi kupitiza viwango hupunguza ufanisi wa kazi kwa mtumishi yeyote.
Akitoa salama za shukrani Mganga Mkuu wa wilaya ya Kyela ndugu Mariam Ngwere amesema, sisi kama watumishi tumeyapokea yote tuliyoelekezwa na kiongozi wetu na tunaahidi kuyafanyia kazi.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa