Kiasi hicho kimetolewa katika semina ambayo ilihudhuriwa na; Mwenyekiti wa halmashauri ya kyela, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya kyela, Afisa maendeleo jamii na viongozi wengine kutoka katika taasisi tofauti pamoja na wajasiliamali kutoka sehemu mbali mbali za wilaya ya kyela tarehe 13/4/2021 ndani ya ukumbi wa mamlaka ya mji mdogo wa kyela, kwaajili ya kuwaendeleza wajasiliamali wadogo wadogo wakiwemo wanawake, vijana na walemavu.
Akizungumza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya kyela ndugu, Ezekiel Magehema katika semina hiyo amesema kuwa, hii sio mgao wa fedha ambayo haitarejeshwa, fedha hii ni mkopo ndio maana tunalazimika kutoa mafunzo kila wakati na kuhakikisha kwamba mikopo inarejeshwa kwa wakati, lengo kubwa ni kuwataka wajasiliamali wakafanye yale yaliyo dhamiliwa kufanya, watengeneze faida na warudishe mtaji wakati huo shughuli zao zikiendelea.
Pia, ndugu mkurugenzi ameongeza kwa kusema, kuna vikundi vilifanya vizuri, na vingine vilifanya vizuri zaidi, hivyo basi kwa vikundi ambavyo vilifanya vizuri zaidi hatukusita kuongeza nguvu zaidi katika vikundi hivyo.
Aidha, mwenyekiti wa halmashauri ya kyela mhe.Kature Godfrey Kingamkono amesema kuwa, faida ya kulipa mapato na ushuru haya ndio matokeo yake, hizi pesa hazijatoka serikali kuu, zimekusanywa kwenye mikokoa, mawese na maeneo mengine yote. Hivyo watendaji wa kata na vijiji wanapokuja kuchukua ushuru tusijenge uadui kwasababu wanafanya hayo kwa faida ya wanakyela.
Mwisho, mwenyekiti alitoa pongezi kwa vikundi ambavyo vilileta bidhaa zao walizo tengeneza kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri wakiwemo walemavu, ambao walitengeneza meza ya miti, na kinywaji kiitwacho Banana wine kutoka kwa wajasiliamali wengine ambacho kina nembo ya kyela, lakini pia kulikuwa na vikundi vya wanawake ambao walifuma mashuka. Pamoja na hayo mafunzo ya mikopo kwa vikundi vya ujasiliamali yaliendelea katika mamlaka ya mji mdogo wa kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa