Mwenge wa uhuru umewasili leo na kukabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase katika viwanja vya shule ya sekondari (KCM) ukitokea Halmshauri ya wilaya ya Rungwe tarehe 28/8/2024.
Mapokezi hayo yameambatana na vikundi mbalimbali vya burudani ikiwemo vijana wa hamasa wilaya ya Kyela, vikundi vya ngoma za asili pamoja na vikundi vya muziki.
Wakizindua mradi wa Barabara kata Mwanganyanga kiongozi wa mbio za mwenge ameipongeza kitengo cha Manunuzi, kwa kutumia mfumo wa manunuzi NeST kwani wamekua msatari wa mbele kuutumia na kuunganishwa na wazabuni mbalimbali ili kufanya manunuzi ya kiserikali.
Vilevile katika uzinduzi wa klabu ya kupinga rushwa katika shule ya sekondari Kyela, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, amewakabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mwanafunzi wenye ulemavu na kugawa vifaa vya kujifunzia, pamoja na vifaa vya michezo kutoka katika ofisi ya Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela.
Pamoja na hayo Ndugu Mnzava, amempongeza Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine manase kwa kuwatunza na kuwashirikisha katika kazi za mikono kama kilimo cha bustani na kuwaweka katika mazingira bora ya kusomea.
Aidha kwa wanafunzi amesisitiza kujikinga na ugonjwa hatari wa malaria unaopelekea idadidi kubwa ya vifo pamoja na kuwataka wananchi kukataa na kupinga vitendo vya rushwa ili kuleta haki katika maisha.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa