Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga, amefungua kikao kazi cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mbeya, leo tarehe 15/04/2024, katika ukumbi wa mikutano wa wilaya ya Chunya.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Chunya Ndugu, Anakleth Michombero, Mratibu wa Mwenge Mkoa, Maafisa mazingira, Maafisa Mawasiliano serikalini, na Waratibu wa Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya
Katika ufunguzi wake Mhe. Mkuu wa wilaya, ameupongeza mkoa wa Mbeya kwa kufanya vizuri katika mapokezi ya mbio za Mwenge za mwaka 2023.
Pia amewataka waratibu kuwa na utaratibu wa kufanya maandalizi mapema ya kuupokea Mwenge wa Uhuru katika wilaya zetu.
Aidha amesema pamoja na miradi tunayoiandaa pia amezitaka halmashauri kuandaa hamasa za kutosha.
Vilevile amesema, ni vizuri kufahamu ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, hasa katika kipengele cha Ujumbe wa Mwenge ambao umebeba suala la mazingira.
Pamoja na hayo, amewataka waratibu kufuatilia mbio za Mwenge kabla hazijafika Mkoani kwetu ili kujifunza na kujiandaa kwa yale ambayo yatokea katika maeneo mengine Mwenge wa Uhuru unapopita.
"Ninaamini tukijiamini, tukijipanga Mkoa wetu unaweza kuwa wa kwanza" amesema Mhe. Mbarak Alhaji Batenga, Mkuu wa wilaya ya Chunya.
Mwisho amewataka waratibu wa Mwenge wa Uhuru kufanya vikao vya tathmini ya mbio za Mwenge katika wilaya zao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa