Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imeitisha kikao cha wadau wa zao la kakao kwa malengo ya kujadiliana juu yakuongeza thamani ya zao kakao Wilayani Kyela. Katika kikao hicho wadau waliomba kuanzishwa kwa vyama vya ushirika, waliomba makampuni yarudi kununua zao la kakao katika vyama vya ushirika. Pia waliomba kuambiwa ni aina gani ya kakao ni nzuri kulimwa ili kupata mazao bora. Nae Afisa kilimo wa Wilaya ya Kyela ndugu P. Sheyo amesema, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr. John Pombe Magufuli kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wameweka mikakati mingi juu ya kuinua zao hili,ikiwemo kuzalisha kwa kutumia ugani, Halmadhauri inaandaa bei dira ya zao hili, kufanya mikutano Mara kwa Mara na wadau wa Kilimo cha Kauai, kikagua magari yanayo beba kakao na utunzaji, uuzaji wa kakao ili kujua uzalishaji halisi katika kijiji kimoja baada ya kingine.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa