Haya yamezungumzwa na wakulima wa zao la mpunga wa kata ya Ngana wilayani Kyela, walipokuwa katika maazimisho ya siku ya mkulima shambani "Fild day" iliyofanyika tarehe 4/12/2018.
Aidha katika maazimisho hayo yalihudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndugu Salome Magambo, ambae alieapongeza wakulima wote waliopata elimu ya kilimo cha umwagiliaji na kueneza elimu hiyo kwa vitendo kwa wakulima wengine.
Pia alisema serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili ya kumsaidia Mtanzania, na ndio maana tunaona serikali imeweka maafisa ugani katika kila kata ili kuwasaidia wakulipa kupata elimu na ushauri wa kilimo vijijini.
Katika msimu wa kilimo mwaka 2018/2019, wakulima 10, kutoka kata ya Ngana walipatiwa mafunzo ya kilimo shadidi cha mpunga, na wakulima hao waliweza anzisha skimu ya kilimo hicho katika kata ya Ngana.
Mwisho wakulima walisifia elimu nzuri waliyoipata kutoka kwa wakulima wenzao waliopata mafunzo na kuleta elimu kwako. Kwani kilimo shadidi kimekuwa ni mkombozi wa matumizi ya maji kidogo, mbegu kidogo na mavuno mengi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa