Mwenge wa uhuru umeridhishwa na utekerezaji wa miradi ya maedeleo katika wilaya ya Kyela, Hili limejidhihirisha wazi baada ya Mwenge wa uhuru kukagua ,kuzindua na kuweka jiwe la misingi katika miradi yote iliyopangwa kupitiwa na mbiyo za mwenge tarehe 11/09/2022 hapa wilayani Kyela.
Kwa mwaka 2022 Mwenge wa Uhuru umezindua miradi mitatu (3), kuwekwa jiwe la msingi miradi mitatu (3) na kukagua miradi miwili (2) yenye thamani ya jumla ya Sh.1,821,851,609.00 ambapo Serikali kuu imechangia Sh 830,000,000.00, Halmashauri Sh.40,980,651.00, Nguvu zawananchi ni shilingi 880,215,000.00 na Wafadhili/Wahisani 70,655,958.00. Miradi hiyo imetekelezwa katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ikimba kitongoji cha Lubele ambao wameshiriki katika mbio hizo za mwenge, kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma amesema, serikali ya awamu ya sita inatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu, amesema hii ni fulsa ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ili kuwanufaisha wananchi wa Tanzania.
Aidha katika kutoa salamu zake Ndugu Sahili N. Nyanzabara amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Ndugu Ezekiel H. Magehema kwa kuwa mbunifu na kutoa mikopo yenye tija kwa wananchi na hadi sasa faida za mikopo hiyo inaonekana kwa macho na wananchi wa Kyela wananufaika na mikopo hiyo na kubadili maisha yao.
Nae Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mery Prisca Mahundi (MB) amesema, anapenda kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Kyela kwa kupata miradi ya vituo vya afya ambavyo vinajengwa dabodabo katika wilaya hii, Alisema jambo hili si la kushangaza katika serikali ya awamu ya sita serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na hayo Mbunge wa jimbo la Kyela alimaarufu mzee wa jumlajumla Mheshimiwa Ally Mlaghila Jumbe amemwambia kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa kwamba, asishangae kuwa kuna baadhi ya sehemu tumeshindwa kuwa sahihi sana kwenye ujenzi, hii inatokana na kuletewa fedha kwa mfulululizo fedha ambazo zimeletwa kwa maombi maalum. Alisema kwa kituo cha afya Njisi yeye aliomba pesa na pesa zilifika mapema sana ndipo waliketi na viongozi wengine ili kujipanga ni sehemu gani wakajenge kituo cha afya, na baada ya majadiriano na Mhe. Mkuu wa Mkoa walikubaliana kujenga kituo hicho cha afya Njisi kwa sababu maalum.
Aliendea kwa kuseama hadi sasa tumejenga vituo vya afya visivyopungua 4 na anategemea baada ya miaka mitano tutakuwa tumejenga vituo vya afya saba katika wilaya ya Kyela.
Mwisho Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa Kyela kwa kuhakikisha wanapata huduma za Kuwekeza katika sekta binafsi. Pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kikusya – Matema KM 39 ambayo imechochea kuleta wawekezaji eneo la fukwe ya ziwa Nyasa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa