Shirika lisilo la kiserikali CRS consenuth kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Kyela, limefanya kongamano yarehe 28/05/2018, katika kata ya Muungano kijiji cha Bukinga wilayani Kyela.
Katika kongamano hilo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo shughuli za utoaji wa chakula cha nyongeza kwa watoto wadogo.
Aidha kongamano hilo lilihudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta. Mkuu wa wilaya ya Kyela alitoa hutuba katika ufunguzi wa kongamano hilo, na aliwaasa wazazi Kuwa na mazoa ya kuwapa watoto wao lishe iliyo bora yaani chakula mchanyato, ili kujenga afya bora za watoto wadogo.
Pia aliwakumbusha wazazi kujipanga katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa watoto punde wanapokuwa shuleni, kwani kwa kumuacha mwanafunzi bila kula kwa mda mrefu ni chanzo kikubwa cha kumfanya mwanafunzi kutofikiri kwa kina.
Mwisho elimu juu ya lishe bora kwa wamama wajawazito na watoto ilitolewa chini ya usimamizi wa Afisa lishe wa Wilaya Bi.Devotha ambae alitoa madhara ya kukusekana kwa lishe bora kwa mama mjamzito.
Alisema magonjwa ya mdomo wazi au kuzaliwa mtoto mwenye ugonjwa wa mgongo wazi si kitu cha ajabu kwani hayo ni madhara anayopata mototo mdogo, toka tumboni mwa mama yake pale mama mjamzito anapokosa lishe bora.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa