Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wa serikali na sekta binafsi wamefanya kongamano kubwa linalohusu utoaji wa taarifa dhidi ya utunzaji wa mazingira wilayani. Kongamano hilo limefanyika tarehe 28/07/2021 Katika ukumbi wa halmashauri.
Akifungua kongamano hilo, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa amesema, Kyela ni wilaya yenye uoto wa asili wa kipekee Sana, hivyo tukizingatia sheria, taratibu na kanuni za utunzani wa mazingira basi kizazi kijacho kitanufaika na mazingira haya, Pia alisema suala la utunzaji wa mazingira ni mtambuka kwani inashirikisha sekta zote zile za serikali na sekta binafsi. Hivyo anaamini washiriki wote baada ya kongamano hilo watakuwa ni mabalozi wakubwa katika utoaji wa elimu dhidi ya utunzaji wa mazingira.
Akiwasirisha taarifa hiyo Afisa maliasili wa wilaya ndugu James Mbaga amesema, jambo kubwa linalowafanya, kuandaa kongomano hilo ni kutaka kuhakikisha kuwa, wadau wa mazingira wanafahamu sheria, taratibu na kanuni za utunzaji wa mazingira na kuzifuata, ili kizazi kijacho kiweze kufaidika na mazingira haya kama sisi tunavyofaidika nayo. Hivyo ni jukumu la jamii nzima kutunza mazingira kwa kushirikiana na asasi za kiraia, Idara na taasisi za kiserikali.
Pia Afisa maliasili huyo aliwataka wajumbe wote wa kongamano hilo, kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kushiriki kampeni za usafi, kudhibiti ukataji hovyo wa miti, kushiriki katika mazoezi ya upandaji miti, kuwa walinzi katika kuzuia mifugo inayozurula hovyo, kuzuia uvuvi haramu, pamoja na kuhamasisha mazingira bora katika viwanda vyetu vya mpunga, mbao, mbosa na vinginevyo ikiwepo na udhibiti wa utupaji wa taka katika mitaro ya kupitishia maji.
Aidha ndugu James Mbaga ameongeza kwa kusema wilaya ya Kyela inakabiliana na ongezeko kubwa la watu, na kusababisha wananchi kutumia kwa fujo maliasili tulizonazo hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.
Wilaya ya Kyela inazalisha tani 10410 za taka kwa mwezi na inauwezo wa kuzoa tani 70 za taka kwa siku. Ili kuongeza shughuli za uzoaji wa taka, Halmashauri ya wilaya imenunua trecka ambalo litasaidia uzoaji wa taka kwa wingi na kuifanya wilaya kuwa safi na Tanzania kwa ujumla.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa