katikati ni Katibu tawala wa wilaya ya Kyela (shati jekundu) kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela (suti) na anaemfuata ni kiongozi wa Kyela ambassadors.
Kiongozi wa Kyela Ambassadors ndugu Aliko Mwaseba, ameongozana na wanachama wa kikundi hicho hadi katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Kyela, leo tarehe 27/04/2020, kwa lengo la kutosha baadhi ya vifaa vitakavyowasaidia wananchi kujikinga na virusi vya corona (COVID-19).
Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na majaba ya maji 6 na sabuni (sanitizer), Akizungumza wakati wa kukaabidhi vifaa hivyo, ndugu Aliko Mwaseba amesema wao kama kikundi wameamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano dhidi ya kupambana na ugonjwa huu, ugonjwa huu umekuwa ni tishio kwa nchi yetu na hata kwa dunia nzima, hivyo wao kama kikundi wameguswa na janga hili hata kufikia maamuzi ya kuchanga na kununua vifaa hivyo vichache ili kuwasaidia wananchi hapa wilayani Kyela.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mhe. Katibu Tawala ndugu Godfrey Kawacha ametoa shukrani zake za dhati kwa kikundi hicho na aliwataka wajumbe wa kikundi hicho kuendelea na moyo huo wa kujitolea, na kwa kufanya hayo watabarikiwa zaidi katika shughuli zao.
Pia aliwataka kuongezeka ili kuwa wengi zaidi katika kikundi chao kwa malengo ya kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa shughuli wazifanyazo. Mwisho alisema, Wanakyela watawaona hamko nyuma katika kuunga mkono jitahida ya kupigana na ugonjwa huu mbaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema ametoa shukrani zake kwa kikundi hicho , kisha akasema:
Kundi hili likawe ni walimu wa kutoa elimu juu ya taratibu ambazo zinatumika pale mgonjwa anapojitokeza katika jamii, yaani kumpleka mgonjwa mwenye dalili za corona katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa haraka.
Pia aliwataka kuzingatia taratibu zote ambazo zimewekwa za kujizuia na virusi vya corona, Na kuzingatia ushauri uliotolewa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kwa kufanya tendo la kujifukiza kwani Corona ni vita.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa