Kyela Cocoa Girls Secondary School, juhudi mahsusi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi makini wa Rais Samia Suluhu Hassan. Shule hii imekuwa mkombozi mkubwa kwa watoto wa kike waliokuwa wakitembea umbali mrefu na hatarishi kusaka elimu katika shule ya sekondari ya Ipande.
Hatahivyo Kyela Cocoa Girls Secondary School ambayo mpaka sasa imegharimu fedha ni Tsh.195,000,000.00/=,kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Tsh. 165,000,000.00 ikiwa ni fedha kutoka mfuko wa Kakao pamoja na Tsh. 30,000,000.00 kutoka tasisi ya Tulia Trust
Kwa miaka mingi, watoto wa kike katika Kata ya Nkokwa na vijiji vya jirani walikuwa wakilazimika kuvuka mapori, vichaka na maeneo yasiyo salama kila siku kwenda Shule ya Sekondary Ipande, hali iliyowavunja moyo wengi na hata kusababisha baadhi ya Wanafunzi kuacha shule. Sasa, kupitia shule hii mpya ya kisasa iliyojengwa jirani kabisa na makazi yao, wanafunzi watasoma kwa amani, usalama na mazingira bora ya kitaaluma.
Ujenzi wa Kyela Cocoa Girls Secondary School umetokana na wazo bunifu na la kizalendo lililoasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Zuberi Homera, kwa kushirikiana kwa ukaribu na Uongozi wa Wilaya ya Kyela . Viongozi hawa waliona umuhimu wa kutumia mapato yanayotokana na zao la kakao kuwekeza moja kwa moja katika elimu ya watoto wa Kata ya Nkokwa
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa