Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna amesema wilaya ya Kyela sio omba omba alipokuwa akizungumza katika hotuba yake, aliyoitoa katika kikao cha Baraza la kufunga mwaka 2017/2018,siku ya jumatano tarehe 19/09/2018, wilayani Kyela.
Amesema, hali ya chakula katika wilaya yetu ni nzuri, kwani uzalishaji wa chakula mwaka 2017/2018 ni tani 94,950, wakati mahitaji ya chakula kwa wilaya ni tani 54,737 kwa mwaka 2017/2018.
Aliongeza kwa kusema wilaya ya Kyela ina chakula cha ziada tani 40,213. Na aliwataka wananchi kutunza chakula chao kulingana na ukubwa wa kaya zao ili kuepukana na balaa la njaa.
Aidha Mhe. Dr. Hunter Mwakifuna alizungumzia miradi ya kimaendeleo iliyofanyika katika wilaya yetu, alisema;
Wilaya ya Kyela ina mtandao wa barabara ya kilometa 556.9, na madaraja 4 yamejengwa, ukarabati wa madaraja 7 umefanyika, makalavati 20 yamejengwa.
Utekelezaji wa haya yote yamegharimu jumla ya shilingi 1,415,235,343.00, na wilaya bado inaendelea kutekeleza miradi 3 ya barabara katika mradi wa kuondoa vikwazo (Bottleneck), ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 3450,391,272 zimetumika.
Aidha katika kukuza na kuinua Tanzania ya uchumi wa viwanda wilaya ya Kyela imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 54.7 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda kwa wananchi wa ndani na wa nje.
Pamoja na hayo, wilaya ya Kyela imeendelea kushirikiana na wadau kama JAICA, TECHNOSERVE, mtenda Rice Supply company limited, GSI, hawa wamesaidia kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi wa wilaya ya Kyela, na hadi sasa Wilaya inaviwanda 245 vidogovidogo vya wajasiriamali hao.
Aidha wilaya ya Kyela imetoa mikopo kwa vikundi 21 kati ya vikundi 54 vya wanawake na vijana, na shilingi 100,000,000 zimetengwa kwa ajiri ya uboreshaji wa masoka yatakayowasaidia wanawake na vijana.
Mwisho aliwashukuru Madiwani na watalaamu wote ambao wameweza na kuthubutu katika swala zima la kusimamia shughuli za maendeleo wilayani Kyela.
Imetolewa na :
Mkurugenzi Mtendaji
Ofisi ya Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa