Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amepokea makombe ya ushindi kutoka kwa wanafunzi walioshiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa leo tarehe 30/5/2024.
Aidhaa Mhe.Mkuu wa Wilaya amewapongeza walimu kwa usimamizi mzuri uliyowawezesha wanafunzi kupata ubingwa, pia ameomba kuzidi kutetea ubingwa huo kila mwaka ili kulinda na kuiwakilisha vyema wilaya ya Kyela.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kyela Bi. Florah Luhala, amewashukuru walimu na wanafunzi kwa juhudi kubwa zilizofanyika ili kuhakikisha ubingwa unarudi kwa mara nyingine hapa wilayani.
Kauli mbiu ya Mitashuta mwaka 2024 ''Miaka Hamsini ya UMITASHUMTA Tunajivunia Mafanikio katika Sekta ya Elimu Michezo na Sanaa, Hima Mtanzania Shiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2024".
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa