Halmashauri ya wilaya ya Kyela imefanya maazimisho ya siku ya wanawake Duniani siku ya tarehe 7/3/2020, maazimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Mafrasop vilivyopo katika kata ya Nkuyu hapa wilayani Kyela, huku mgeni rasmi akiwa ni Mhe. Claudia U. Kitta Mkuu wa wilaya ya Kyela.
Akitoa hutuba yake mbele ya hadhara, Mkuu wa wilaya, aliwataka Wananchi wa wilaya ya Kyela kuazimisha siku ya wanawake kwa amani na pia siku hii itumike katika kuibua fulsa mbalimbali zitakazowasaidia wanawake kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini.
Pia aliwataka wanawake kuwa mfano wa kuigwa katika jamii, hasa katika swala la mavazi na tabia kwa ujumla, kwani watoto wamekuwa wakiiga matendo yote yatendwayo na wazazi wao.
Aidha Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajiri ya wanawake, vijana na walemavu yaani mfuko wa (WDF) na (VWF), kwa lengo la kuyayatoa makundi hayo katika umaskini mkubwa, na Halmashauri ya wilaya ya Kyela imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 80.
Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kizazi Cha Usawa Kwa Maendeleo Ya Tanzania Ya Sasa Na Baadae".
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa