Halmashauri ya wilaya ya kyela imefanya maombolezo Kwaajili ya aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt.John Pombe Magufuli; Maombolezo hayo yamefanyika tarehe 24/3/2021, uwanja wa mwakangale uliopo katika wilaya ya kyela. Maombolezo hayo yamehudhuliwa na wananchi, taasisi za kiserikali na binafsi huku mkuu wa wilaya ya kyela akiwa ni mgeni rasmi wa maombolezo hayo.
Akizungumza mkuu wa wilaya ya kyela Claudia Kitta, amesema kuwa kifo cha Dkt. John Pombe Magufuli kimetuletea simanzi kubwa sio kwa Tanzania tu na dunia nzima maana alikuwa ni Rais wa wanyonge, mpenda haki lakini pia mcha Mungu ambaye alitenda kazi zake kwa kumwogopa Mungu.
Licha ya hayo aliongeza kwa kusema kuwa hayati John Magufuli amegusa sekta zote zikiwemo elimu bila malipo, ujenzi wa vituo vya afya, hospitali mbali mbali nchini, ujenzi wa viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege, miundombinu kila Kona zikiwemo barabara, meli katika maziwa yetu na bahari, na kyela tukiwa miongoni mwa watu walionufaika kwa kupatiwa meli ndani ya ziwa nyasa na kuifikisha Tanzania katika maendeleo ya juu.
Aidha, mwenyekiti wa halmashauri ya kyela ndugu Kature Godfrey Kingamkono alipewa nafasi ya kuzungumza kwenye maombolezo hayo, naye alisema kuwa John Pombe Magufuli alipenda kuamini Mungu, lakini pia kazi pamoja na ukweli na alimalizia kwa kuwataka wananchi wa kyela waendelee kumuenzi hayati John Pombe Magufuli kwa kuwa ameacha alama kubwa ya utendaji kazi wake katika taifa letu.
Mwisho, wananchi waliendelea kama ilivo kuwa kawaida kusaini katika kitabu cha maombolezo kilicho kuwa kimewekwa ndani ya uwanja wa mwakangale kwa siku hiyo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa