Sifa hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albart Chalamila alipokuwa akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wilayani Kyela tarehe 13/08/2018.
Mhe. Albert Chalamila alipongeza viongozi wa wilaya ya Kyela hasa waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Hunter Mwakifuna, kwa jitihada kubwa za kumaliza migogoro iliyokuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wilaya.
Pia alialiwataka viongozi kuachana na tofauti za kiitikadi kwa sasa na kuungana pamoja kwa kusimamia maendeleo kwa wafaida ya wilaya na wananchi kwa ujumla.
Aidha alisema wilaya ya Kyela imekuwa ikijitegemea kwa asilimia 7tu ambapo si kitu kizuri kwa wilaya.
Kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, Halmashauri imekusanya mapato kwa asilimia 67.18 ya mapato yote, na alisema hali hii si zuri na hailidhishi kabisa.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa alisema, inawezekana upungufu wa mapato haya umetoka na changamoto mbalimbali ikiwemo kushuka kwa asilimia ya ushuru wa mazao, hivyo basi ni jukumu la Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato visivyowaumiza wananchi.
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa mkoa wa Mbeya aliipongeza wilaya ya Kyela kwa kupata hati inayolidhisha kwa Mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Mwisho aliwaonya wafanyakazi wazembe kufanya kazi kwa kujituma. Kwani kufanya kazi kwa kupapasa ni kutokuitendea haki Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na aliwasii kubadilika haraka kwani hatua za kinidhamu zitachukuliwa haraka kwa wafanyakazi wasiotaka kubadilika.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa