Haya yamezungumzwa leo tarehe 03/02/2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera, alipokuwa akifanya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti, zoezi lililofanyika katika viwanja vya shule Mpya ya sekondari Njisi iliyopo kata ya Njisi wilaya ya Kyela.
Amesema kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya, wazee maarufu, mashirika na wadau wa mazingira tunao uwezo mkubwa wa kuifanya wilaya ya Kyela kuwa ya kijani kwa kupanda miti kila mahali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma zuberi Homera akizungumza na wananchi kabla ya zoezi la upandaji miti.
Aidha Mheshimiwa Homera amesema ameamua kuja kufanya uzinduzi wa upandaji miti, ili kuhamasisha jamii kupanda miti, na baada ya uzinduzi wa zoezi hili, kila mwanafunzi atatakiwa apande miti 5, kisha tupande miti katika maeneo ya Zahanati, Hospitali ya wilaya pamoja na kwenye vituo vya afya. Na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetimiza agizo la Makamu wa Rais Mheshimiwa Mhe. Dkt. Philip Isidori Mpango.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera akipanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti wilayani Kyela.
Katika suala la miundo mbinu, Mhe. Homera, amewaambia wanaKyela kuwa mkandarasi yupo njiani kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Njisi Itungi port ikiwa na taa za barabarani. lakini pia amewataka wananchi kuendelea kusimamia mpango mzuri wa matumizi ya ardhi kwa maendeleo yao.
Aidha alitoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwa kuikumbuka Kyela, na hata kuwajengea vituo vingi vya afya, pamoja na shule mpya nyingi ambapo wananchi na wanafunzi wameendelea kuapata huduma. Amesema kwa wanafunzi 5236 wa Mkoa wa Mbeya, waliokosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza, watapelekwa katika vyuo vya ufundi ili kupunguza watoto wa mtaani, majina ya wanafunzi hao yatatolewa.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Keenja Manase akizungumza na wananchi wa kata ya Njisi kabla ya zoezi la uzinduzi la upandaji wa miti wilayani Kyela.
Nae Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Keenja Manase, amewataka viongozi wa wilaya ya Kyela, kuendelea kushirikiana ili kuendeleza zoezi la upandaji miti katika wilaya yetu ya Kyela.
Mheshimiwa Josephine Keenja Manase Mkuu wa wilaya ya Kyela, (kulia) akipanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa upandaji miti katika wilaya ya Kyela.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi diwani wa kata hiyo Mhe. Omary Mwijuma amesema, maendeleo yanayoonekana leo ni nguvu ya serikali ya inayoongozwa na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, leo hii tunayaona madarasa ya kisasa kwenye kila shule.
Halmashauri ya wilaya ya Kyela imeweza kuitumia siku ya upandaji miti kwa kupanda miti 300, ikiwemo miti ya matunda, vivuli, mapambo na michikichi.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa