Maadhimisho ya siku ya mwanamke yamefanyika tarehe 07/03/2023, katika kata ya Busale kijiji cha Lema hapa wilayani Kyela.
Maadhimisho hayo yameambatana na maonyesho ya kazi mbalimbali kutoka katika vikundi vya wajasiriamali pamoja na shuhuda za vikundi vilivyofanikiwa kubadili maisha yao ya umaskini hadi kuwa na maisha ya kawaida, baada ya kupata mikopo isiyokuwa na riba kupitia Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Keenja Manase amesema;
Amefurahishwa na maandalizi mazuri ya siku ya mwanamke yaliyofanyika katika kata ya Busale, ambayo yamejaa shangwe na bashasha kubwa.
Aidha ametoa shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuijenga Tanzania pamoja na kumuokoa Mtanzania hususani mwanamke pamoja na makundi maalum kwa kutoa mikopo isiyokuwa na riba.
Pamoja na hayo Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka wazazi kuwa mfano wa kuigwa katika familia zao na amekemea tabia za kupenda ngono, ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya, kwani kwa kuacha tabia hizo, wazazi wanaweza pata muda wa kukaa na familia zao na kuzifundisha matendo mema.
Nae Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi mkoani Mbeya ndugu, christiner Msiyani amesema,
Anapenda kuwatia moyo wanawake wote kusimama kifua mbele, kwani wapo wanawake wenzao katika jeshi la polisi, wanaosimamia sheria bila kupindisha, hivyo wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa za unyasaji na ukatili wa kijinsia muda wowote wanapokutana na changamoto hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela, Ndugu Ezekiel H. Magehema, ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuikumbuka wilaya ya Kyela, kwa kuleta fedha nyingi ambazo zimeibua miradi mingi ya maendeleo ambayo ni msaada mkubwa katika kutoa huduma kwa wananchi na kuwaletea maendeleo yao binafsi.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa