Siku ya vijana huadhimishwa kila tarehe 12/08 kila mwaka, ikiwa na lengo la kuwakutanisha vijana ili kuweza kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maslahi yao.
Hapa Wilayani Kyela maadhimisho haya yamefanyika katika shule ya Sekondari Kajunjumele Kata ya kajunjumele, na katika maazimisho hayo Elimu ya ujasiliamali, elimu dhidi ya maambukizo ya UKIMWI, na mimba za utotoni zilitolewa na wawezeshaji mbalimbali.
Aidha Afisa Maendeleo wa Wilaya ndugu Missani amewataka vijana kuanza kufanya mambo yaliyomema katika jamii na kuachana na makundi maovu, hasa yale yanayotumia madawa ya kulevya, kwani serikali ya awamu ya tano inamalengo mazuri ya kuwawezesha vijana hasa wale wanaojitambua.
Mwisho alisema vijana wanapaswa kujitambua, kuheshimu na kuthamini kazi zinazofanywa na serikali yetu, kwa mfano, utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne, kutoa mikopo kwa wanawake na vijana, utoaji wa bima za Afya.
Serikali inayafanya haya kwa lengo la kuwa na Wananchi wenye kujitambua na kujielewa wakiwa na afya bora.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa