Mafunzo ya watendakazi wa NTDs yaani watenda kazi wa umezeshaji wa dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, yanafanyika leo tarehe 17/11/2022 katika ukumbi wa Kanisa la Morovian makabulini Kyela, Mafunzo haya yameshirikisha walimu wa shule za msingi, wahudumu kutoka kada ya Afya pamoja na waratibu elimu wa tarafa ya Unyakyusa.
Mafunzo haya yanatolewa na TOTs, na yamebeba maudhui ya jinsi ya kujikinga na magonjwa yasipewa kipaumbele, Magonjwa hayo ni kama, Kichocho na minyoo ya tumbo na Usubi, Mafunzo haya yanafanyika ili kijiandaa kwenda kutoa dawa ya kinga tiba kwa wanafunzi wa waliopo shuleni na wale wasiokuwepo shuleni wenye umri usiopungua miaka 5 hadi 14.
zoezi hili linakwenda kufanyika hapa wilayani tarehe 22/11/2022 na 23/11/2022.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa