Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela Mheshimiwa Emmanuel Bongo akifungua kikao cha Baraza katika ukumbi wa mamlaka ya Mji Mdogo Kyela.
Mamlaka ya Mji Mdogo Kyela Yapitisha rasimu ya bajeti ya shilingi 520,051,000/= kwa mwaka wa fedha 2022/2023, bajeti hii imepishwa katika kikao cha Baraza la mamlaka hiyo, kikao kilichofanyika tarehe 10/01/2022.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kyela (mualikwa) Mhe. Gelvance Ndaki amesema,
Anapenda kutoka salamu za Chama Cha Mapinduzi(CCM), na amesema Chama kinawatakia kikao chema.
Aidha amewaasa wajumbe wa kikao katika suala hili la upitishaji wa bajeti kwamba,
Chama kinawataka wajumbe wa kikao kuzingatia Ilani ya Chama ili malengo ya kuwaleta maendeleo wananchi yaweze kutimizwa kama ilani ya Chama inavyotutaka kutekeleza.
Aidha alisema anategema bajeti hii inakwenda kumgusa kila mwananchi.
Kwani Baraza hili ni sehemu ya chombo cha kuzungumzia maendeleo ya mamlaka kwa ujumla wake, Jambo la muhimu ni kuzingatia vipaumbele vyenye manufaa kwa maendeleo ya wilaya na Nchi.
Nae Mwenyekiti wa baraza hilo Mheshimiwa Emmanuel Bongo, alitoa shukrani zake za dhati kwa watumishi na viongozi kwa jinsi wanavyoshirikiana katika kufanya kazi, na aliwaomba wenyeviti kuitisha mikutano na wananchi wao kwa kila mwezi katika vitongoji vyao, ikiwa ni mojawapo ya majukumu ya viongozi katika kuleta maendeleo ya vitongoji hivyo na wilaya kwa ujumla.
Mwisho Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo ndugu Gerald Mlelwa aliwashukuru wajumbe wa Baraza hilo kwa kukubali na kuridhia kupitisha rasimu ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa