Haya yamezungumza na Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe. Joseph Kandege alipokuwa akifunga maazimisho ya maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Mwakangale Jijini Mbeya.
Amesema maonesho ya Nanenane mwaka huu wa 2018 yamefana sana ukilinganisha na miaka mingine. Kwani watu wamejitokeza kwa wingi sana na wengi wao ni wajasiliamali wa viwanda vidogo vidogo.
Aidha Mhe. Naibu Waziri amewasisitiza watalamu kuzidi kufanya tafiti dhidi ya technolojia ya viwanda ili kuweza kifikia malengo na dira ya nchi yetu kuelekea uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2025.
Pia alitoa maagizo kwa Halmashauri zote kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajiri ya kilimo.
Aidha aliwataka Wananchi wote walifika katika maonesho haya, kufikisha elimu hii hadi vijijini walipo wakulima.
Kwa upande wa vijana mhe. Aliwaasa vijana kujiunga katika vikundi ili kuweza kujipatia mikopo mbalimbali.
Mwisho akiagiza secta za Serikali na secta binafsi kufikisha habari za umuhimu wa kilimo kwa Wananchi wote nchini.
Mkuu wa wilaya ya Kyela (katikati)Mhe.Claudia U. Kitta akiwa katika maonesho ya nanenane
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa