Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amezindua zoezi la ugawaji miche 11,081 ya kokoa kwa Wakulima 125 wa kata mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kyela katika ofisi za Idara ya Kilimo za Halmashauri tarehe 20.2.2025.
Akizindua zoezi hilo Mhe.Mkuu wa Wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali Wananchi wake kuleta Kilimo cha kisasa kitakachowainulia kipato.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amewapongeza Wakulima walionufaika na miche hiyo pia amewataka kuitunza vizuri kupitia Elimu waliopata kutoka kwa Wataalamu wa Kilimo.
Aidha Mhe Josephine Manase amesema kokoa ni zao la kimkakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwani kupitia tozo ya Tsh 20 kwa Kilo moja kwa wanunuzi wa Zao hilo ni kwaajili ya Afya, Elimu Pamoja na Kilimo.
Mhe.Manase amewaagiza Wataalamu wa kilimo kutembelea wakulima wa awali waliochukua miche hiyo na kujua maendeleo ya uzalishaji wao ili kutoa hamasa kwa Wananchi wengine waweze kuzalisha Zao hilo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Bi.Florah A .Luhala amewataka wakulima wa kokoa na wananchi kwa ujumla kuwafichua Watu wanaosafirisha zao la Kokoa katika Halmashauri jirani bila yakufuata utaratibu.
Kwa upande wao Wanufaika wa Miche hiyo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na uongozi wa Wilaya kwa kuwawezesha kupata miche ya kisasa itakayowasaidia kupata mavuno kwa wingi na kujikwamua Kiuchumi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa