Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Bi.Lydia Herberty amezindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Wilaya katika Uwanja wa Kipija Arena tarehe 22.02.2024.
Akizindua mashindano hayo Kaimu Mkurugenzi amesema Michezo ni sehemu ya ajira pamoja na Kuimarisha Afya hivyo amewataka Wachezaji wanaoshiriki Michezo hiyo kufanya juhudi zaidi ili waweze kufikia malengo yao.
Aidha Kaimu Mkurugenzi amewasihi wanafunzi hususani washiriki wa Michezo kufuata maelekezo wanayopewa na Walimu wao wa Michezo ili waweze kupata ushindi utakaowawezesha kushiriki UMISSETA ngazi ya Mkoa na Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Wah. Madiwani Mhe. Gwakisa Mwakipesile amemshukuru Nabii Sanga kwa kudhamini mashindano hayo yenye tija katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwani kupitia Mashindano hayo Wanafunzi wanapata fursa ya kuimarisha afya Pamoja na kujenga urafiki baina yao.
Kwa upande wake Mdhamini wa Mashindano ya UMISSETA ngazi ya Wilaya Nabii Sanga ameahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Fedha Taslim, Ng'ombe,Jezi pamoja na traki suti ili kuhamasisha kufanya vizuri zaidi kwa ngazi ya Mkoa na Taifa.
Vilevile Afisa Michezo Wilaya ya Kyela Ndg. Zephania Jumbe amewaomba Walimu wa Michezo wa shule zote kujenga ushirikiano mzuri baina yao ili waweze kupata timu bora ya Wilaya itakayokwenda kuwakilisha na kushiriki mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa