Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Ndg. Keneth Nzilano amefungua mashindano ya UMITASHUMTA kwa ngazi ya Wilaya yaliofanyika katika viwanja vya Kipija Alena tarehe15.2.2025.
Akifungua mashindano hayo Kaimu Mkurugenzi amewapongeza Walimu wa shule zote za msingi kwa kuandaa timu zitakazoweza kushiriki mashindano hayo.
Aidha Kaimu Mkurugenzi amewasihi wanafunzi kufuata maelekezo wanayopewa na walimu wao ili waweze kuwa wachezaji wazuri na waweze kufika ngazi ya Mkoa na Taifa.
Vilevile mdhamini wa Mashindano hayo Ndg. Godlove Mwakibete amewataka Wanafunzi hao kuzingatia Masomo wanayofundishwa na Walimu Shuleni na kuamini katika Vipaji walivyonavyo.
Kwa upande wake Afisa Michezo Wilaya ya Kyela Ndg. Zephaniah Jumbe amesema mashindano hayo yatasaidia kupata timu bora itakayoenda kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa