Haya yamezungumzwa leo tarehe 04/08/2018 na Mhe. Claudia U. Kitta, alipokuwa akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu za miti na viriba vya kupandia miti katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Mbegu za miti pamoja na viriba vya kupandia miti, vimetolewa kwa asasi mbalimbali zikiwemo asasi za KABAO, asasi ya Ikombe, asasi ya Kasumulu pamoja na shule ya sekondari Itope.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya amezitaka vikundi vyote ambavyo vimepata mbegu hizo na viriba, kuwa ni mabarozi wa kwenda kuwaelimisha wananchi kufika katika bustani ya Halmashauri na kujipatia miche ya miti ili kwenda kupanda miti hiyo na kutunza mazingira yetu.
Katika mwaka huu wa 2018, Halmashauri ya wilaya ya Kyela imepanda miti isiyopungua 1500 katika eneo la darajani Boda, ilihali utunzaji wake umekuwa mdogo sana.
Mwisho Mhe. Mkuu wa wilaya alimshukuru meneja wa TFS ndugu James Wumbura kwa kutoa mbegu za miti na viriba vya kupandia miti ili kuweza kutunza mazingira yetu, huku akiwataka wadau wote kupanda miti hiyo umbali wa mita 60 kutoka katika kingo za mito.
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia U. Kitta akihakiki mbegu za miti zilitotolewa leo
Imeandaliwa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa