Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, imeanza kutoa mafunzo ya bima ya afya (CHF) iliyoboreshwa Kwa mda wa siku tatu kwa wafanyakazi wa Afya zaidi ya 130.
Wafanyakazi hao ni pamoja na Wauguzi wa zahanati, wenyeviti wa uendashaji wa vituo, waganga wafawidhi wa kila kituo na mjumbe mmoja wa Afya kutoka kila kituo cha Afya.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi ndugu F. Mwaipopo amesema, mafunzo haya yanalengo ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa Afya, ili waweze kutoa elimu kwa umma na Wananchi kwa ujumla juu ya mfuko wa bima ya Afya iliyoboreshwa.
Aidha Kaimu Mkurugenzi alisema Selikali ya awamu ya tano imeamua kutoa mafunzo haya, ili kuwajengea uwezo watumishi wa afya ambao kwa sasa watapokea fedha za uendashaji wa mfuko huu moja kwa moja katika vituo vyao vya afya na zahanati, ikiwa ni tofauti na njia ya upokeaji fedha katika hospitali ya wilaya.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Dr. Marium Ngwere amesema, watumishi wa Afya watajifunza maswala ya upangaji bajeti, usimamizi wa fedha, kufanya tathimini ya fedha na kufanya maboresho ya changamoto ya bima ya zamani.
Aidha bima ya afya (CHF) iliyoboreshwa itamsaidia mteja kupata huduma za kiafya ndani ya Mkoa. Ikiwa ni tofauti na bima ya mwanzo ambayo mteja aliruhusiwa kupata huduma za kiafya ndani ya wilaya tu.
Hivyo basi Serikali imeona ni vema kutoa elimu kwa watumishi wake, na elimu hiyo isadie katika kutoa huduma bora za bima ya afya iliyoboreshwa.
Mwisho kaimu Mkurugenzi alifungua mafunzo hayo kwa wataalamu, pia alimuagiza Kaimu mganga Mkuu kutoa taarifa kwa wajumbe wote ambao hawata hudhulia.
Ili aweze kuwabaini na kujua chanzo cha kuto kuhudhulia mafunzo hayo na hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa watakaobanika kukaidi mafunzo hayo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa