Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameongoza maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani ambayo katika Mkoa wa Mbeya yamefanyika Halmshauri ya Wilaya ya Kyela kiwanja cha Kipija Arena tarehe 7.3.2025.
Miongoni mwa waliohudhuria maadhimisho hayo ni pamoja viongozi wa Halmshauri mbalimbali za Mkoa wa Mbeya,Wanawake na Wasichana wa Taasisi na Idara, Wanafunzi, Wananchi wa Wilaya tofauti ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Maadhimisho hayo yamesindikizwa na vikundi mbalimbali vya burudani ikiwemo vikundi vya nyimbo, vikundi vya ngoma,pamoja na mitindo ya mavazi ya aina tofauti.
Akizungumza katika maadhimisho hayo.
Mhe.Homera
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwajali wanawake na kuwaletea mradi wa jengo la mama na mtoto linalosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Mhe. Juma Zuberi Homera amewapongeza wanawake na waliohudhuria sherehe hiyo,pia amewataka kutumia siku hiyo kwa kutiana hamasa katika shughuli mbalimbali zitakazowainulia kipato.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaasa wanawake kuwa na ushirikiano mzuri na wenza wao hususani katika malezi na misingi iliyo bora ili kujenga na kuandaa kizazi imara kwa maslahi Taifa hapo baadae.
Aidha, Mhe.Homera amewataka wanawake kuondokana na adha inayosema" WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA"na kutumia kaulimbiu inayosema WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE HAKI USAWA NA UWEZESHAJI.
Awali Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mikopo ya 10% inayosaidia wanawake wengi kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.
Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amesema maadhimisho hayo ni chachu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanyika na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pia ni fursa ya kubadilishana kupata mawazo mapya yatakayosaidia wanawake hao kujijenga kiuchumi.
Kaulimbiu "WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE HAKI USAWA NA UWEZESHAJI."
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa