Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe leo tarehe 31/10/2023 amegawa Pikipiki 4 kwa vikundi 4 vya bodaboda hapa wilayani Kyela.
Vikundi vilivyogawiwa ni kikundi cha bodaboda njia panda Kapwili kata ya Bondeni, kikundi cha bodaboda njia panda ya Ipinda, kikundi cha bodaboda Kalumbulu pamoja na kikundi cha bodaboda katika hospitali ya wilaya ya Kyela.
Aidha amegawa mifuko 100 ya saruji katika shule ya sekondari Lubele ili kusaidia ujenzi wa miundo mbinu ya shule, bando 4 za bati katika ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Talatala, mifuko 100 katika mradi wa maji kambasegela.
Pamoja na kukabidhi vitu hivyo Mhe. Mlaghila amesema Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ofisi ya Mbunge imesadia ujenzi wa Zahanati ya Kingili kwa kutoa fedha Tsh.1,000,000/= na saruji mifuko 50, Kusaidia ujenzi wa matundu 14 ya vyoo katika shule ya msingi Kyijila kata ya Nkokwa, Saruji mifuko 200 kwa ujenzi wa kituo cha afya Itope.
Si hayo tu bali Ofisi imesaidia ununuzi wa mafuta katika kituo cha polisi Tshs. 5,000,000/=, uboreshaji wa kiwanja cha mpira Ikombe shs.2,000,000/=, ununuzi wa compyuta na "printer"
Ofisi imetoa Tshs 2,750,000/= kusaidia ujenzi wa kituo cha afya Ngereka kata ya makwale, ofisi imesaidia Tshs 2,000,000/=, kikundi cha kutengeneza batiki Tuganene, ununuzi wa taa za barabarani pamoja na mambo mengine mengi.
Mhe. Ally Mlaghila Jumbe amesema, amegawa hivi vitu kwa sababu ya nguvu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani, maana bila nguvu yake asingeweza kuyafanya hayo, hivyo wanaKyela hatuna budi kumshukuru Mhe. Rais.
Mwisho amesema vitu hivi vyote vinatolewa ikiwa ni ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa wilaya ya kyela, akiwemo Mhe. Mkuu wa wilaya, Baraza la madiwani, Mkurugenzi na wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa