Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, leo tarehe 28/05/2024, amefanya ziara ya kutembelea na kukagua, miradi ya maendeleo katika kata ya Nkokwa na Busale.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameongozana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Kyela, pia baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka halmashauri.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa shule ya Kokoa Girls na Mradi wa shule ya wasichana ya Mkoa wa Mbeya katika kata ya Busale.
Akiwa katika kata ya Nkokwa Mhe. Mkuu wa wilaya, amewataka wanaNkokwa kusimamia mradi wa shule ya Kokoa Girls, kwa nguvu zote ili kuhakikisha mradi unatekelezwa na unakamilika kwa wakati.
Amewataka viongozi kushikamana ili kuijenga kata yao, Pia kuleta maendeleo yenye tija. Pamoja na hayo, amewaomba viongozi kuwashirikisha wananchi ili waweze kusaidiana katika kukamilisha mradi, vilevile amezitaka kamati zinazohusika na ujenzi kuhakikisha vifaa vyote vya ujenzi vinapatikana kwa wakati ili kutokukwamisha maendeleo ya mradi.
Aidha amemtaka mtendaji kata, kutoa taarifa kwa wananchi, ikiwemo taarifa za mipango za uendelezaji wa kata, pia kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya miradi yote inatekelezwa katika kata yao.
Nae diwani ya kata ya Nkokwa Mhe. Luka Mwakitalu amemshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya kwa kutembelea mradi wa shule ya Kokoa Girls, kwani ujio wake umeongeza chachu ya kutekeleza mradi kwa kasi kubwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa