Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kijiji cha Kabanga kata ya Katumbasongwe tarehe 09/09/2024.
Ziara hiyo imeambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri, Bi. Flora A. Luhala, Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya Mhe. Katule G. Kingamkono, wataalam kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Akisikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kabanga ikiwemo suala la ujio wa nabii kwa ajili ya kufanya Ibada ya maombi katika kijiji chao, Mhe.Mkuu wa wilaya amesema"
Kwa mujibu wa taratibu na sheria ya nchi ya Tanzania viongozi wa dini wanapaswa kuwa na vibali maalum vitakavyowatambulisha ili waweze kufanya huduma zao pasipo usumbufu, Pia amesisitiza wananchi hao kua na imani thabiti kupitia dini na madhehebu yao ili kujiepusha na utapeli wa kidini.
Aidha katika suala la mpasuko wa mto Songwe unaoleta usumbufu wakati wa mafuriko Mhe.Josephine Manase, amewaomba viongozi wa kata ya Kabanga, kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kupanda miti itakayosaidia kuzuia mafuriko ikiwemo upandaji wa magugu, matete na mianzi pia.
Vilevile amewaomba wananchi wa kijiji cha Kabanga, kulinda na kutunza vyanzo vya maji kwa kusitisha shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo shughuli za kilimo katia vyanzo vya maji.
Sambamba na hilo Mhe. Mkuu wa wilaya, amewaomba wananchi kujiepusha na tabia ya uuzaji wa mazao shambani, pia amesisitiza wakulima kuweka taratibu ya bei rasmi ya mazao ili kuepusha tabia ya unyonyaji kwa wakulima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Mhe .Katule G. Kingamkono, amewaomba wananchi kijiji cha Kabanga kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi wao katika suala la udhibiti wa mpasuko katika mto Songwe, unaoleta uharibifu mkubwa wa mazingira wakati wa masika.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa