Leo tarehe 12/10/2021 Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule G. Kingamkono, ameanza ziara ya kutembelea baadhi ya Kata hapa wilayani.
Lengo la ziara zake ni kuendeleza shughuli za kuhamasisha maendeleo katika kata na wilaya kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti ameweza kukutana na wananchi wa kata ya Busale, na kutoa pongezi kwa Mhe.Diwan Kabeta na wananchi kwa kuanzisha miradi mingi ya maendeleo, Pongezi pia zilitolewa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mbunge, Mkurugenzi na watalaam.
Amesema, ili tupate maendeleo ni lazima wananchi wajifunge mkanda, kwani hakuna jambo zuri linalokuja bila maumivu. Pia amewaambia kuwa Serikali Kuu imeleta pesa kiasi cha Shilingi Mil. 25,000,000/= kwa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya sekondari Busale, hivyo, amewataka wanaBusale kuzisimamia pesa hizo na kuzidisha nguvu ya kuchanga michango kwa kutekeleza miradi mbalimbali iliyoanzishwa katika kata hiyo. Ziara hizi zitaendelea
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa