Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono amefanya ziara katika shule za Sekondari Kyela na Makwale, kwa lengo la kukagua na kujua changamoto za ujenzi wa madarasa, ziara hii imefanyika tarehe 28/12/2020 hapa wilayani Kyela.
Aidha katika kutembelea madarasa hayo Mwenyekiti aliweza kufanya vikao vifupi na wadau wa maendeleo katika maeneo hayo.
Akiwa katika kikao katika shule ya sekondari Nyasa amesema, anaishukuru kampuni ya ununuzi wa kakao Bioland na Kim's chocolate, kwa mchango wao wa dhati na hata kusababisha madarasa haya yanajengwa kwa kasi kubwa.
Pia aliwaomba wenyeviti na madiwani husika katika kata kutoka na kwenda kwa wananchi kuomba michango ili kufanikisha ujenzi huu wa madarasa, kwani wao kama viongozi wamejipanga katika kuwatumikia na kufanya kazi kama timu ili kuibadili wilaya ya Kyela kimaendeleo.
Mheshimiwa mwenyekiti amewaambia wadau wa maendeleo kuwa, Kyela tumekuwa nyuma sana katika kuchangia vitu vya msingi, kwa sasa ni vizuri kujenga utamaduni wa kushirikiana na kuchangia maendeleo kwa kila kata , kwani madarasa na maendeleo ya miundo mbinu hii itatumika na wanafunzi wanaotoka hata nje ya kata hizi na sehemu mbalimbali za nchi kuja kusoma hapa Kyela.
Nae katibu wa mbunge wa jimbo la Kyela ndugu Edga Mwasamlagila, amesema ni vizuri kwa awamu inayokuja tusikimbizane mwishoni kwa ujenzi wa madarasa ni vyema kujiandaa mapema, Kwani ofisi ya Mbunge ipo bega kwa bega na wnanchi katika ujenzi wa madarasa wakati wowote.
Shule ya sekondari Kyela kwa sasa wapo katika ujenzi wa vymba vitatu vya madarasa ikiwa ni kupunguza uhaba wa vyumba saba vinavyotakiwa kujengwa, na shule ya sekondari Makwale wao wanajenga vyumba vinne vya madarasa.
Mwisho viongozi waliwapongeza walimu kwa kazi nzuriJuhudi za walimu tumeziona na ndio maana kuna ongezeko la ufaulu mzuri.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa