Wazee maarufu na wastaafu wakiwa wamejipanga katika kuanza mdahalo katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Kyela. Ikiwa ni maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru Tanzania Bara.
Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yameadhimishwa kwa kishindo hapa wilayani Kyela, maadhimisho haya yalianza tarehe 01/12/2022 hadi kufika kilele tarehe chake 09/12/ 2022.
Katika wilaya ya Kyela maadhimisho haya yameshirikisha wananchi kwa kufanya usafi wa mazingira, Mahojiano mbalimbali yaliyohusu maendeleo ya Nchi kabla na baada ya uhuru, upandaji wa miti katika mazingara, Michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa zawadi kwa washidi wa michezo, Na kuhitimishwa kwa kupitia Mdahalo mkubwa uliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela tarehe 09/12/2022.
Akitoa hotuba yake Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa SACP. Ismail Mlawa amesema, wilaya ya Kyela ni wilaya iliyozaliwa kutoka katika wilaya ya Rungwe mwaka 1972, baada ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuanza kujitegemea katika nyanja mabalimbali za kimaendeleo.
Pamoja na hayo Mhe. Mkuu wa wilaya amewakumbusha wananchi kuwa, Sherehe hizi za miaka 61 ya Uhuru ni wakati wa kujitafakari, tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Hivyo aliwataka wananchi kushirikiaana na Serikali yao inayoongozwa na Dr. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujikita kufanya maendeleo ya WILAYA ya Kyela, kwani maendeleo yanaanza na Sisi wenyewe.
Wilaya ya Kyela kwa miaka 61 ya Uhuru imeweza kufanya maendeleo mengi sana kwa wananchi wake, "Mafanikio haya yalianza tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere hadi kipindi hiki cha awamu ya sita kinachoongozwa na Dr. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Amesema Mhe. Mlawa.
Wananchi wilayani Kyela wakiwa ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya wilaya tayari kwa kuanza mdahalo wa miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Pia amesema, Wilaya ya Kyela imepata maendeleo makubwa katika secta zote muhimu ikiwemo, Kilimo, Afya, Elimu, Maji pamoja na miundo mbinu.
Akizungumzia suala la elimu, Mheshimiwa Ismail Mlawa amesema, kabla ya Uhuru wilaya ya Kyela ilikuwa na shule za msingi 18 tu, lakini baada ya miaka 61 ya Uhuru wilaya ya Kyela imekuwa na shule 112 za msingi, Aidha hakukua na shule ya sekondari kabla ya Uhuru ila kwa sasa kuna shule za sekondari 31na shule 6 zikiwa ni za binafsi, maendeleo yaliyopatika kwa kasi ya ajabu.
Kwa upande wa afya Mheshimiwa Mkuu wa wilaya amesema, wilaya ya Kyela kabla ya uhuru ilibahatika kuwa na kituo cha Afya 1 ambapo kwa sasa ndiyo hospitali ya wilaya, ila baada ya Uhuru Kyela imekuwa na Hospitali 3, vituo vya afya 5 zahati 41 pamoja na cliniki10.
Aidha aliendelea kusema kwamba, kwa upande wa miundo mbinu wilaya ya Kyela imepiga hatua kubwa kwa kutengeneza barabara za lami zenye kilometa 56.8, barabara za changalawe kilometa 75.6 pamoja na barabara za udongo kwa kilometa 435.19 kiwango ambacho huwezi fananisha kabla ya miaka 61 ya Uhuru.
Katika suala la umeme Mheshimiwa malawa amesema, wilaya ya Kyela kwa sasa imefanikiwa kuwa na umeme wa uhakika na wilaya imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwa kata zote 33, vijiji 58 pamoja na vitongoji 176 katika wilaya aidha ameendelea kusema kuwa, Ni vijiji 35 pekee vilivyobakia kwa kutokuwa na umeme wilayani Kyela, Na vijiji 19 vitawashwa umeme hivi karibuni na Vijiji vilivyosalia 16 mpaka Februari 2023 vitakuwa vimefikiwa na umeme. Ambapo kabla ya uhuru huduma ya umeme haikuwa ya uhakika katika wilaya yetu.
Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu, Ezekiel H. Magehema alitoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu maadhimisho haya kuafanyika katika kila wilaya, amabapo yamesababisha wananchi kukutana na kijadiliana kwa pamoja mambo muhimu ya maendeleo. Pia ametoa shukrani zake za dhati kwa wazee wote waliohusika katika mdahalo, waandaaji pamoja na vyombo vya habari vikiwemo Keifo Fm pamoja na Baharia online Tv kwa ushiriki wao mzuri.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyasa English Medium wakiwa wanasakata rumba kabla ya kuanza mdahalo wa maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa