Shukrani Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miaka yako 3 Wanakyela tumeyaona mengi kutoka kwako;
Tumepokea shilingi 6,018,180,028 kupitia Idara ya Elimu Sekondari fedha zilizotumika kujenga madarasa 81, shule 2 mpya, lakini pia tunaendelea na ujenzi wa shule 1 kubwa ya kidato cha I hadi VI, kukarabati maabara katika shule 4, umaliziaji wa maboma ya madarasa na kujenga nyumba za walimu. Tumefanikiwa kuongeza shule 6 kutoka idadi ya shule 22 hadi 28, ambapo zaidi ya wanafunzi 1528 wamepeta nafasi ya kuendelea na masomo hali ambayo bila shule hizo idadi ya wanafunzi 1528 huenda wangekosa nafasi ya kuendelea na masomo.
Vilevile Mheshimiwa Rais ametupa kiasi cha shilingi 2,292,424,000 kupitia Idara ya Elimu msingi ambazo zimejenga shule 2 mpya za msingi madarasa 98 baadhi yake yamejengwa upya na mengine yamekarabatiwa, matundu 95 ya vyoo, bweni, vituo vya walimu katika kata 4, na kuwasaidia wanafunzi 5915 kuendelea na masomo pamoja na ongezeko la ajira kwa walimu.
Aidha katika Idara ya Afya tumepokea 4,850,000,000 fedha zilizojenga zahanati 3 mpya, kituo cha afya 1, Jengo la ghorofa kwa matumizi ya Mama na mtoto jengo linalojengwa katika Hospitali ya wilaya, vifaa tiba, nyumba ya watumishi wa 3, Maendeleo haya yamekwenda kusaidia zaidi ya wananchi 6915 kupata huduma bora za afya ndani ya wilaya ya Kyela.
Aidha shilingi Bilioni 20.9, tumepewa kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa skimu ya Makwale, ikiwa jumla ya shilingi 66,287.028 tumepokea na kuanzisha mradi wa kupanda miche ya chikichi na kakao ambapo wananchi wilayani Kyela wananufaika kwa kugawiwa miche bure, fedha hizo pia zimesaidia kuanzia shughuli ya utotoleshaji wa vifaranga vya samaki na utoaji wa chanjo kwa mifugo ya wananchi.
Pamoja na hayo shilingi Bilioni 6.7 tumepewa ili kusaidia kutengeneza na kurekebisha miundombinu ya barabara, ambapo kwa sasa tunazo barabara za lami hadi katikati ya mji wetu wa Kyela, ikiwa ni pamoja na kufungua barabara za vijijini na kumfanya Mwanakyela kufunguka katika shughuli za kujipatia kipato na kukua kiuchumi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa