Haya yamezungumzwa na mratibu wa mradi wa usimamizi endelevu wa ardhi ya bonde la ziwa Nyasa ndugu. Aswile Fumbo katika kikao kilichofanyika jana tarehe 7/06/2018.
Kikao hicho kilihudhuliwa na watalamu wa mazingira kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela pamoja na Asasi mbalimbali, lengo ikiwa ni kupeana majukumu ya kulinda mazingira ya bonde la ziwa Nyasa.
Maradi huu ulizinduliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais tarehe 10/hadi tarehe 11/08/2017 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Kwa mwaka huu mradi utagharimu shilingi milioni 47,144,000/= kwa kufuata vipengele vikuu vitatu yaani uzinduzi, uibuaji na kuanzisha mradi.
Mradi huu ni mtambuka kwa karibu sekta nyingi zikiwemo, Kilimo, Maendeleo ya jamii,Ardhi na Mali Asili, Uvuvi Mazingira, Habari na baadhi ya sekta zinazojikita pale zinapohitajika.
chini ni picha za baadhi ya wadau wa mradi huu wakichangia mawazo yao katika kikao hicho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa