Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase akipanda mti ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine Manase ameshiriki katika zoezi la upandaji miti, tarehe 08/12/2023, katika viwanja vya shule mpya ya Ibanda sekondari ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za miaka 62 za Uhuru wa Tanzania Bara.
Akiwa katika zoezi la upandaji miti Mhe. Mkuu wa wilaya, amewataka wananchi kuendelea kumuomba mwenyezi Mungu ili aendelee kuilinda amani tuliyonayo na kuishi kwa upendo tulionao kama waasisi walivyotuachia amani ya kweli katika nchi yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Frolah Luhala akipanda mti katika eneo la shule ya mpya ya sekondari Ibanda.
Amesema pamoja na kazi ya kupanda miti ambayo inaacha alama ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara, pongezi nyingi zimetolewa kwa kamati ya usimamizi wa mradi wa shule ya sekondari Ibanda kwa usimamizi mzuri na kumaliza mradi kwa wakati.
Aidha amewapongeza wanaIbanda kwa kujitoa katika kufanya kazi mbalimbali kwenye mradi wa shule mpya ya sekondari Ibanda.
Amewataka wananchi wa kata ya Ibanda kurudisha fadhira na kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani ameupiga mwingi katika kutuletea fedha nyingi zinazotekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya yetu.
Pia ametoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi. Frolah Luhala na timu yake kwa usimamizi mzuri wa mradi wa shule ya Ibanda.
Wilaya ya Kyela umetekeleza maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru Tanzania bara kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti isiyopungua 70,000.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa