Haya yamezungumzwa leo tarehe 14/11/2022 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono alipokuwa akifungua mafunzo kwa vikundi 10 ambavyo vitapewa mkopo wa shilingi 110,000,000/=.
Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema, Halmashauri ya wilaya ya Kyela imekuwa ikitoa mikopo kwa vikindi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kila robo ya mwaka, kwa hiyo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutambua kuwa mikopo ya Halmashauri inatolewa kwa wananchi kwa kufuata taratibu na sheria ambazo zimewekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kusaidia wananchi wake.
Aliendelea kwa kusema, Masuala ya utoaji wa mikopo yapo kisheria na ndio maana Serikali iliweka sheria ya kutoa mikopo yenye tija ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini na kujikwamua katika hali ya umaskini.
Pamoja na hayo, Mheshimiwa Katule amewaweka wazi wanavikindi kwa kuawaambia kuwa, fedha hizi zimetokana na mapato ya ndani ya Halamashauri, ambayo yamekusanywa na wataalam wetu wakisimamiwa na kiongozi imara Mkurugenzi Mtendaji ndugu Ezekiel H. Magehema hivyo ni lazima tuwapongeze lakini pongezi nyingi ziende kwa wananchi wenyewe ambao ndio walipa kodi.
Aidha aliwaasa wanabikundi kuwa na umoja mara baada ya kupata mikopo, na kuepuka migogoro. "Duniani kusingekuwa na migogoro basi hata hapa tulipo tungekuwa tupo paradiso" alisema Katule Kingamkono.
hivyo aliwaasa vikundi kuepuka migogoro na wajenge umoja na ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuongeza mawazo chanya ya kutanua mitaji wanayoipata kwa kupitia mikopo hii, ili kupata mafanikio katika maisha, na kutambua thamani ya mikopo hii inayoenda kutolewa na Halamashauri ya wilaya ya Kyela.
Pia alivitaka vikundi kujifunza kuweka akiba kwani akiba hiyo itakuja kuwasaidia pale wanapokwama, lakini kupunguza matumizi yasiokuwa ya lazima.
"Utajiri sio Ushirikina, Matamanio ya viongozi ni kuona mwananchi wa chini ananufaika na Serikali yao" ailisema Katule.
Aidha ameahidi kwamba kwa kikundi chochote ambacho kitafanya vizuri katika marejesho na kupiga hatua ya maendeleo kwa mwaka, basi Halmashauri itakikopesha kikundi hicho shilingi 50,000,000/= ili kukiendelee kufanya vizuri na kuwa na mafanikio zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake Grolia M. mwakibange ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wananchi wote wa kipato cha chini ili kwa kupitia mikopo hii waweze kujiinua na kuongeza kipato katika familia zao.
Mwisho
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa