Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela akiwa katika mradi wa ujenzi wa darasa katika shule ya sekondari Kajunjumele.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Ezekiel H. Magehema amefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, ziara iliyofanyika tarehe 05/11/2021, miradi inayotekelezwa na pesa ya UVIKO 19 iliyoletwa na Serikari ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania ili kupunguza upungufu wa vyumba vya madarasa hapa wilayani Kyela.
Fundi ujenzi akiwa kazini katika ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya sekondari Kajunjumele.
Akiwa katika ziara yake, Ndugu Magehema amepata fulsa ya kukagua baadhi ya miradi ikiwemo, mradi wa chumba 1 cha darasa katika shule ya sekondari Kajunjumele, Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya sekondari Ngonga, ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya sekondari Ikolo, pamoja na ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Ngonga.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amewataka wasimamizi ngazi ya kata kuandika na kutunza vizuri nyaraka zote zinazotumika katika zoezi zima la ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Ezekiel H. Magehema(tisheti ya bluu) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wasimamizi wa ujenzi katika shule ya sekondari Ikolo.
Pia amewataka viongozi wasimamizi kuwahimiza mafundi ili kukimbizana na muda uliopangwa kea ajiri ya ukamilishaji wa miradi hiyo. Pamoja na hayo amekumbusha suala la kufuata taratibu za manunuzi ya vifaa vya ujenzi na alitoa pongezi kwa kasi inayokwenda kwa baadhi ya miradi inayoendelea.
Mkurugenzi Mtendaji akiwa katika mradi wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya sekondari Ngonga.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa